Wakipsigis

Askari Wakipsigis miaka ya 1950.

Wakipsigis ni jina la kabila dogo ambalo huhesabiwa katika kabila kuu la Wakalenjin, ambao ni miongoni mwa Waniloti wa Nyanda za Juu nchini Kenya. Wanachukua sehemu kubwa ya bonde la ufa nchini humo.

Wanaishi hasa katika kaunti za Bomet, Kericho na Nakuru. Hata hivyo kutokana na maendeleo ya jamii na uchumi wanapatikana sehemu mbalimbali nchini Kenya na hata nchi za nje.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy